Sunday 5 February 2017

AFCON 2017:CAMEROON WON THE FIFTH AFCON CUP IN FRONT OF EGYPT

CAMEROON YATWAA TAJI LA KOMBE LA MATAIFA AFRICA(AFCON2017) KWA MARA YA TANO BAADA YA KUICHAPA MISRI 2-1

Usiku wa February 5 ndio siku ambayo mchezo wa fainali ya mataifa ya Afrika maarufu kama AFCON 2017 ulichezwa,  mchezo wa fainali ya AFCON 2017 ulikuwa unazikutanisha timu za Misri dhidi ya Cameroon, lakini Cameroon wamefanikiwa kufuta uteja kwa kufungwa fainali mbili.
d caption
Cameroon wamefanikiwa kutwaa taji la AFCON 2017 kwa mara ya tanobaada ya kupata ushindi wa goli 2-1 zidi ya misri ambayo ndio ilitangulia kupata bao kupitia kwa mchzaji wake wa kimataifa ambaye anaichezea club ya Arsenal Mohammed Elnely, katika dakika ya 20 tu ya mchezo, matumaini ya cameroon yaliibuka baada ya Nicolas N’koulou kufunga goli la kusawazisha katika dakika ya 58,Vincent Aboubakar mshambuliaji wa Basiktas ndio alizima ndoto za Misri baada ya  kufunga goli la ushindi katika dakika ya 88 ya mchezo
.
ushindi huo unakuja baada ya Cameroon kufumgwa fainali mbili za AFCON na Misri, alifungwa fainali ya AFCON 2008 goli 1-0 Mohamed Aboutrika akifunga goli hilo, lakini walipoteza fainali ya AFCON 1986, Cameroon wanakuwa wamechukua taji lao la tano laAFCON wakati Misri wanabakia na rekodi yao ya kuchukua mataji nane ya AFCON.

Saturday 4 February 2017

MATOKEO YA CHELSEA Vs ARSENAL HAYA HAPA

CHELSEA YAFUNGA ‘KIDOMODOMO’ CHA ARSENAL KWA 3-1 KUELEKEA UBINGWA WA EPL

Image result for matokeo kati ya chelsea vs arsenalChelsea imepanda point 12 juu ya kilele cha ligi ya Uingereza EPL baada ya kuinyamazisha Arsenal. Marcos Alonso aliiweka kifua mbele Chelsea baada ya kufunga kwa kichwa kufuatia shambulio la Diego Costa.
The Blues baadaye waliongeza bao la pili dakika saba baada ya muda wa mapumziko baada ya Eden Hazard kuchenga safu ya ulinzi ya Arsenal na kufunga kwa urahisI. Mchezaji wa zamani wa Chelsea Cesc Fabregas alimaliza udhia baada ya kipa Ceck kuifanya masikhara na kumpatia mpira wa bure.

Image result for olivier giroud scoring chelseaHata hivyo mshambuliaji wa Arsenal Oliver Giroud alifunga bao la kufutia machozi kwa niaba ya Arsenal katika dakika za mwisho za mechi.

Thursday 2 February 2017

MICHEZO


CAMEROON KUKIPIGA NA MISRI FAINALI YA AFCON BAADA YA KUICHAPA GHANA 2-0
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjxaVapeASGjCOqxMpV9L4REGMdpGhyrgMPqEGGyYKvOIOD3Mpwy06DSBXpAcT20zZ0qUFF9B5aul5NE5AOBP1I265jYdv_k9MOz2s82zsIdUH9p0-b1RVNxQ2ehWXVk2vbyTa3H6L3wnc/s1600/Cameroon.jpeg
Timu ya taifa ya Ghana usiku wa February 2 2017 inaungana na timu ya taifa ya Burkinafaso kuiga michuano ya AFCON 2017, hivyo inatokana na kukubali kipigo cha goli 2-0 kutoka kwa timu ya taifa ya Cameroon katika mchezo wao wa nusu fainali ya pili ya AFCON.        Magoli ya Cameroon yalifungwa na Michael Ngadeu dakika ya 72 kabla ya Christian Bassogog kuzima ndoto za Ghana kucheza fainali dakika za nyongeza, ushindi huo unaifanya Cameroon kutinga fainali ya AFCON 2017 na watacheza na fainali dhidi ya Misri, fainali ambayo itakuwa inajirudia ya mwaka 2008 ambapo Misri alimfunga Cameroon kutwaa taji lake la sita.