Saturday 4 February 2017

MATOKEO YA CHELSEA Vs ARSENAL HAYA HAPA

CHELSEA YAFUNGA ‘KIDOMODOMO’ CHA ARSENAL KWA 3-1 KUELEKEA UBINGWA WA EPL

Image result for matokeo kati ya chelsea vs arsenalChelsea imepanda point 12 juu ya kilele cha ligi ya Uingereza EPL baada ya kuinyamazisha Arsenal. Marcos Alonso aliiweka kifua mbele Chelsea baada ya kufunga kwa kichwa kufuatia shambulio la Diego Costa.
The Blues baadaye waliongeza bao la pili dakika saba baada ya muda wa mapumziko baada ya Eden Hazard kuchenga safu ya ulinzi ya Arsenal na kufunga kwa urahisI. Mchezaji wa zamani wa Chelsea Cesc Fabregas alimaliza udhia baada ya kipa Ceck kuifanya masikhara na kumpatia mpira wa bure.

Image result for olivier giroud scoring chelseaHata hivyo mshambuliaji wa Arsenal Oliver Giroud alifunga bao la kufutia machozi kwa niaba ya Arsenal katika dakika za mwisho za mechi.

3 comments:

  1. Wanazidi kuongeza gape tu..coz cjelsea now ana point 59 wakati tot ana 47points tofauti ya point 12 kati yao
    ..

    ReplyDelete